Mapokezi ya uchangamfu
Wahudumu wetu watakupokea, kukuelekeza na kukusaidia kupata sehemu nzuri ya kukaa.
Karibu Nyumbani
Iwe ni mara yako ya kwanza kututembelea au umejiunga nasi kupitia mtandaoni, tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu katika T.A.G Mwenge Christian Centre.
Tutafurahi kukuona
Wahudumu wetu watakuwa tayari kukupokea na kukuongoza, kuanzia kukusaidia kupata sehemu ya kukaa hadi kuwaelekeza watoto wako kwenye madarasa yao maalumu.
Ibada zetu ni mikusanyiko yenye maombi, sifa na kuabudu, kwaya na Neno la Mungu. Tunakusanyika kumwabudu Mungu na kukua pamoja katika imani yetu ndani ya Yesu Kristo.
Utakachokutana nacho
Tumeandaa mazingira ya kukusaidia wewe na familia yako kushiriki ibada kwa utulivu.
Wahudumu wetu watakupokea, kukuelekeza na kukusaidia kupata sehemu nzuri ya kukaa.
Watoto wa miaka 2–15 wanapata nafasi salama ya kujifunza Neno la Mungu, umisheni na uwakili wa Kikristo.
Tarajia muda wa maombi, kusifu na kuabudu, huduma ya kwaya na mafundisho ya Neno la Mungu.
Jumapili hii
Karibu ushiriki nasi katika ibada ya wiki hii. Mungu akubariki sana.