← BackTAG Mwenge Christian Centre

Wanawake Watumishi wa Kristo

Wanawake wanaomcha Mungu ni jeshi kubwa.

WWK inawajenga wanawake katika imani, maombi, upendo na huduma ili wawe mashujaa wa Kristo katika familia, kanisa na jamii.

Wanawake Watumishi wa Kristo TAG Mwenge
Jina Rasmi la IdaraWWK · Wanawake Watumishi wa Kristo
Andiko la IdaraMuhubiri 9:10a
Rangi za IdaraNyekundu, Nyeupe

Wito wa mwanamke

Mwanamke wa imani huleta tumaini.

Mungu anamwita kila mwanamke kuwa shujaa wa imani: kusimama katika kweli, kuziombea familia na kuwafikia wengine kwa upendo wa Kristo. Kama wanawake mashujaa tunaowaona katika Biblia, mwanamke wa leo anaweza kutumia imani, hekima na maombi kuleta mabadiliko katika kizazi chake.

WWK ni sehemu ya wanawake kukua katika Neno la Mungu, kuimarishana na kutumikia pamoja. Tunatamani kuona wanawake na watoto wao wakimjua Kristo, wakisimama imara na kuwa nuru katika familia, kanisa na jamii.

Ushirika wa wanawake wa WWK TAG Mwenge
Ushirika, umoja na huduma
01

Shujaa wa imani kama Esta

Esta alisimama kwa unyenyekevu, maombi na ujasiri kwa ajili ya watu wake. Mwanamke wa Mungu naye huitwa kusimama katika pengo na kuombea familia, kanisa na taifa.

Esta 4:16
02

Hekima ya Debora na Yaeli

Debora na Yaeli walitumia hekima, uamuzi na uwezo waliopewa na Mungu. Mfano wao unatukumbusha kuwa Mungu humtumia mwanamke kuleta ushindi na kulinda kizazi chake.

Waamuzi 4:4–9, 21
03

Kuombea uzao wetu

Wanawake wanaitwa kuwaombea watoto wa kike na wa kiume, kuwafundisha kweli ya Mungu na kuwaongoza wamjue Yesu Kristo na kuishi katika wokovu.

Mithali 22:6
04

Kuvaa silaha zote za Mungu

Maisha ya imani yana mapambano ya kiroho. Kwa kweli, haki, imani, wokovu, Neno la Mungu na maombi, mwanamke anaweza kusimama imara ndani ya Kristo.

Waefeso 6:10–18

Pamoja tunaweza

Simama, omba na litumikie kusudi la Mungu.

Kila mwanamke ana nafasi ya kutumia vipawa vyake, kuimarisha familia yake na kushiriki Injili. Tukiwa wamoja katika Kristo, tunaweza kuwafikia wanawake wengine, kuwaleta watoto kwa Yesu na kulijenga kanisa kwa upendo na huduma.

“Bwana analitoa neno lake; wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa.”Zaburi 68:11