Mpende Mungu na familia yako
Upendo wa kweli unaonekana katika kujitoa, kuheshimu, kusikiliza na kuitunza familia. Baba anaitwa kuipenda familia yake kwa mfano wa upendo wa Kristo.
Waefeso 5:25Christian Men's Fellowship
CMF inawajenga wanaume kumjua Mungu, kuongoza kwa mfano na kuwajibika katika familia, kanisa na jamii.

Je, wewe ni baba?
Baba anayemcha Mungu anajua utambulisho wake ndani ya Yesu Kristo na huishi kama kielelezo cha imani nyumbani. Wanaume wamepewa nafasi ya kujenga familia zao kwa upendo, uaminifu na hekima inayotokana na Neno la Mungu.
Upendo wa kweli unaonekana katika kujitoa, kuheshimu, kusikiliza na kuitunza familia. Baba anaitwa kuipenda familia yake kwa mfano wa upendo wa Kristo.
Waefeso 5:25Uongozi wa kiroho unaanzia nyumbani. Jenga familia kwa kusoma Neno la Mungu, kushuhudia, kuomba pamoja na kufanya maamuzi yanayomheshimu Mungu.
Yoshua 24:15Baba awajibike kwa mahitaji ya familia yake kwa bidii, uaminifu na moyo wa kutoa, huku akimtumaini Mungu kama chanzo cha mahitaji yote.
Wafilipi 4:19Baba bora hujenga mazingira ya rehema. Kusamehe, kuomba msamaha na kurejesha mahusiano huleta uponyaji na umoja ndani ya familia.
Mathayo 6:14Maisha mapya
Ndani ya Kristo, mwanaume anaweza kuanza upya, kukua kiroho na kuijenga familia yake katika kweli, upendo na tumaini.
“Mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.”Yoshua 24:15